Latest News & Events

 • Tangazo Muhimu kwa wanachuo wa mwaka wa pili 2019 (updated 05/02/2019)
  Kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 11/02/2019 kutakua na mafunzo kwa wanachuo wa mwaka wa pili kuhusu mtaala wa elimu ya awali, darasa la kwanza na la pili na darasa la tatu hadi la sita, hii ikiwa ni sehemu ya programu ya maandalizi ya ufundishaji kwa njia ya vitendo (BTP). Hivyo wanachuo wote wa mwaka wa pili ambao likizo yao iliisha tarehe 27/01/2019 wanatakiwa kuhudhuria mafunzo haya muhimu na ya lazima, ambaye hatahudhuria mafunzo haya hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoruhusiwa kushiriki mafunzo kwa vitendo (BTP).

  Imetolewa na Uongozi wa Chuo.

 • Tahadhari kwa wanachuo wote (updated 05/2019)

 • Siku za karibuni kumekua na taarifa za kupotosha zinazosambazwa kupitia njia ya ujumbe wa simu za mkononi zikitaarifu wanachuo mambo mbalimbali ikiwemo wanachuo wa mwaka wa kwanza kutakiwa kurejea chuoni, tunapenda kuwataarifu kuwa ujumbe wowote unaosambazwa kupitia namba za simu ambazo si rasmi kama vile uongozi wa chuo, mhasibu au mkufunzi wa chuo zipuuzwe. Kama mlivyoelekezwa, endapo utapokea ujumbe wowote kuhusu taarifa za chuo kwa namba ambayo haifahamiki na si ya uongozi wa chuo, mhasibu au mkufunzi tafadhari toa taarifa mapema kwa uongozi wa chuo. vile vile mnashauriwa kutumia tovuti hii na akaunti rasmi ya facebook ya chuo http://www.facebook.com/Mhondatc kupata taarifa rasmi kadri zinavyotolewa.

 • Wajibu Mkuu wa Mwalimu (na TSD)
  Tume ya utumishi ya walimu (TSD) iliwahi kutembelea chuo chetu na kutuelimisha pamoja na mambo mengine mengi, wajibu mkuu wa mwalimu

  Soma zaidi »

For Prospective Students

To apply for the studies at our college please visit NACTE .

Apply via NACTE Admision System »

Sare za Wanachuo