Maelekezo Muhimu kwa Wanaotarajia kujiunga

Our college offers opportunity to join teachers training to all persons from all over Tanzania. The qualifications for the one who wishes to apply and send application are as follows, -Must have at least a form four certificate with division three at one sitting (first priority will be given to those who have credits in Mathematics, Science subjects and English).

MwadiliKaribu sana katika kurasa huu wa idara ya usajili ya Chuo Cha Ualimu Mhonda.Hapa utapata taarifa mbalimbali muhimu kwa wanachuo wapya na wanaotarajia Chuo Cha Ualimu Mhonda..

Kwa kuchaguliwa kujiunga na Mafunzo ya ya Ualimu Elimu ya Msingi/Awali hapa chuoni kwetu, ni nafasi ya pekee kwako kwani wengi hawakubahatika kuipata. Ni matumaini yetu kwamba ufikapo hapa Chuoni utatumia nafasi hii vizuri. Chuo cha Ualimu Mhonda kipo katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Mvomero, Tarafa ya Turiani, Kata ya Mhonda, Kijiji cha Mhonda. .Ni umbali wa kilometa 104 kutoka Morogoro mjini, na kutoka Turiani hadi Chuoni ni umbali wa kilometa 3 .

Uthibitisho wa Afya

Unapaswa kupimwa afya yako kabla ya kufika Chuoni na daktari yeyote wa Hospitali inayotambuliwa na Serikali. Iwapo utakuja bila uthibitisho wa daktari udhuru wowote hautapokelewa. Kama unatumia dawa maalum kulingana na maradhi yako uje dawa zako. Aidha, Chuo kinatoa huduma ya kwanza tu. Unatakiwa kupakua Fomu ya kupimwa afya yako kwa kubofya hapa

Namna ya Kufika Chuoni

Ufikapo kituo cha Morogoro (Msamvu) Panda basi linaloelekea Turiani mojawapo ni; B.M -Coach, ZENJIBAR, MSUYA, ZEELAND , au gari ndogo za Noah n.k. Nauli yake Tsh. 5000/ tu. Ufikapo Turiani teremka katika kituo cha Soko la ndizi chukua usafiri kuelekea Chuoni nauli ya pikipiki ni Tsh 1500/= hadi 2000/= tu aidha zipo Noah za kukodi kwa gharama ya Tsh. 10,000/= NB:Unatakiwa kufika Chuoni kabla ya saa 12.00 jioni.

Ulipaji Ada na Michango Mbalimbali

Ada ilipwe kwenye akaunti Na 22010000456 jina la A/C ni UCHANGIAJI ADA ZA CHUO MHONDA, katika benki ya NMB.

Michango yote ilipwe kwenye akaunti Na: 22001100005 jina la akaunti MHONDA T.C. katika benki ya NMB.

Pesa taslimu haipokelewi chuoni . Fedha za matumizi binafsi zisiwekwe kwenye akaunti hizo kwani zitakuwa mali ya chuo na hazitarudishwa, ni vema mwanachuo akafungua akaunti yake binafsi au akatunza kwenye simu yake kama anayo.

Unapofika Chuoni utatakiwa kutoa risiti mbili za malipo za malipo ya ada na michango kama ilivyofafanuliwa katika fomu ya maelekezo ya kujiunga (joining instuructions) amabayo unaweza kuipakua kwa kwa kubofya hapa

  Sare Rasmi za Wanachuo

Kusajiliwa Chuoni

Mara ufikapo Chuoni pitia hatua zifuatazo ili uweze kusajiliwa:-

 • Onana na mlinzi ili upate maelekezo
 • Onana na Msajili wa Wanachuo ili uwasilishe, vyeti halisi na nakala zake. Vyeti hivyo ni
 • (a) Cheti cha kidato cha nne (Academic Certificate)
 • (b) Cheti cha kidato cha sita (kwa aliyehitimu)
 • (c) Vyeti cha kuhitimu shule( leaving certificate)
 • (d) Cheti cha kuzaliwa
 • (f) Cheti cha ndoa (kwa aliyenacho)
 • (iii) Onana na Mhasibu/Msarifu wa Chuo ili ukabidhi risiti za ada na michango uliyolipia Benki.
 • (iv) Onana na Boharia ili kukabidhi vifaa.
 • (v) Onana na Mratibu Taaluma ili upangiwe darasa.
 • (v) Onana na Mwadili wa wanachuo ili upangiwe bweni.
 • NB: Chuo hakitampokea Mwanachuo atakayekuja bila:
 • (a) vyeti vyote halisi (original) na vivuli vyake vilivyotajwa hapo juu.
 • b) Kutokamilisha ada michango yote hautasajiliwa.
 • Aidha, Kwa wale wanaofadhiliwa na mashirika waje na vithibitisho vyao vyenye saini na muhuri wa Shirika/Wizara/Idara husika.

  Kwa yeyote atayebainika ana vyeti visivyo halali hatua kali itachukuliwa dhidi yake ikiwa pamoja na kupelekwa Polisi mara moja

  MOTO WA CHUO ELIMU ILETE USAWA.

  DIRA YA CHUO KUAANDAA WALIMU BORA WENYE MAADILI WANAOJALI JINSIA HAKI NA WAJIBU

  WITO WA CHUO: MWALIMU KUWA CHANZO CHA MABADILIKO CHANYA KITAALUMA, KITAALAMU NA KIMAADILI KWA KUCHOCHEA UBUNIFU, UDADISI NA UTAFITI.

  Taarifa Muhimu

  Pakua joining Instructions 2018/2019

  Medical Examaination Form